Arsenal yaangukia Olympiakos wakati Man u wakikabana na AC Milan katika Europa league 16 bora

Arsenal kwa mara nyingine tena imepangwa pamoja na mabingwa wa Ugiriki Olympiakos kwa tika awamu ya 16 bora kuwania kombe la Europa League kwa mjibu wa droo iliyoandalwia Ijumaa alasiri.

The Gunners wataanzia Athens kabla ya kumalizia nyumbani London.

Katika mechi nyingine vigogo wa Uingereza Manchester United wataanzia nyumbani Old Traford dhidi ya AC Milan ya Italia, ikiwa mara ya kwanza kwa mshambulizi Zlatan Ibrahimovic kurejea Manchester tangu ahame.

Ajax ya Uholanzi imepangwa dhidi ya Young Boys ya Uswizi , Dynamo Kyiv ya Ukraine ichuane na Villarreal ya Uhispania ,As Roma kutoka Italia ikumbane na Shakhtar Donetsk ya Ukraine .

Dinamo Zagreb kutoka Croatia itakuwa na miadi dhidi ya Tottenham ya Uingereza Tottenham ,Slavia Praha kutoka Jamhuri ya Czech imenyane na Rangers ya Scotland huku
Granada ya Uhispania ikihitimisha ratiba dhidi ya Molde ya Norway.

Mikondo ya kwanza itasakatwa Machi 11 huku marudio yakiwa Machi 18 mwaka huu ikifuatwa na mechi za kwota fainali baina ya April 8 na 15 nazo nusu fainali zipigwe kati ya April 29 na Mei 6 nayo fainali ichezwe mjini Gdansk Poland tarehe 26 Mei .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *