Anthony Joshua kuzichapa dhidi ya Kubrat Pulev Desemba 12

Mwingereza Athony Joshua atashuka ulingoni Desemba 12 mjini London  kupigana dhidi ya Kubret Pulev wa Bulgaria kuwania taji ya dunia katika uzani wa Heavy.

Pigano hilo litakuwa bila mashabiki ukumbini,ingawa promoter anatafakari kuweko na idadi ndogo ya mashabiki .

Joshua, hajapigana tangu Desemba mwaka jana alipopigana Andy Ruiz huku pia akitazamiwa kumenyana na  Tyson Fury mwaka ujao .

Joshua aliye na umri wa miaka 31 amepigana mara 24 kushinda mara 23 ,ikiwemo mara 21 kupitia Knock out na kupoteza moja .

Kwa upande wake Pulev aliye na umri wa miaka 39 ,amepigana mara 29 kushinda 28 ,ikiwemo 14 kwa njia ya Knockout na kupoteza pigano moja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *