Amos Nyaribo aapishwa kuwa gavana wa Nyamira

Amos Nyaribo ameapishwa kuwa gavana wa pili wa kaunti ya Nyamira.

Nyaribo ambaye amekuwa naibu gavana wa kaunti hiyo anachukua wadhifa huo kufuatia kifo cha gavana John Nyagarama tarehe 18 mwezi huu.

Nyaribo aliapishwa na jaji wa mahakama kuu ya Nyamira Esther Maina.

Hafla hiyo ya kufana iliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Nyamira ilihudhuriwa na wageni kadhaa mashuhuri akiwemo waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa na magavana kadhaa wakiongozwa na  mwenyekiti wa baraza la magavana aliye pia gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya.

Akimpongeza gavana huyo mpya, Wamalwa alimwambia gavana Nyaribo kwamba watu wa Nyamira na wakenya kwa jumla wanatarajia mengi kutoka kwake na akaelezea matumaini kwamba gavana Nyaribo atajitahidi kuleta maendele zaidi katika kaunty hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *