Aliyekuwa waziri nchini Congo DRC ahukumiwa kwa ulanguzi wa fedha

Waziri wa zamani katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kosa la ulanguzi wa fedha na uhamishaji wa fedha kutoka nchi hiyo hadi ngámbo kinyume cha sheria.

Viongozi wa mashtaka walimchunguza Willy Bakonga kuhusiana na wizi wa fedha zilizonuiwa kugharimia mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi  nchini humo.

Bakonga alirudishwa nyumbani kutoka nchi jirani ya Congo-Brazzaville mwezi uliopita, ambako alikamatwa alipokuwa akiabiri ndege kuelekea mji mkuu wa Ufaransa, Paris akiwa na kiasi cha dola 30,000 za kimarekani kwenye mkoba wake.

Mnamo mwezi wa Februari, Benki ya Dunia ilisitisha utoaji wa kitita cha kwanza cha msaada wa jumla ya  dola milioni 100 kwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kugharimia mpango wa elimu bila malipo kutokana na hofu ya ufisadi.

Mwezi uliopita, maafisa wawili wa elimu ya umma walihukumiwa vifungo vya miaka 20 gerezani kwa wizi wa fedha za serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *