Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Buyoya ahukumiwa kifungo cha maisha

Mahakama ya juu nchini Burundi imemhukumu kifungo cha maisha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Buyoya kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mrithi wake Melchior Ndadaye.

Buyoya  ambaye ana umri wa miaka sabini, kwa sasa ni mjumbe wa muungano wa Afrika katika eneo la Sahel.

Hajawahi hudhuria vikao vya kesi hiyo ambayo mwaka uliopita aliitaja kuwa inayochochewa kisiasa.

Aidha watu wengine 15 wengi wao maafisa wa zamani wa jeshi pia walihukumiwa vifungo vya maisha huku makamu wa rais wa zamani Bernand Busokoza alihukumiwa kifungo cha miaka 20.

Mwaka wa 2018, Burundi ilitoa kibali cha kimataifa cha kukamatwa kwa  Buyoya, ambaye aliongoza taifa hilo mara mbili kutoka mwaka wa 1987 hadi mwaka wa  1993 na pia kutoka mwaka wa  1996 hadi mwaka wa 2003.

Anasemekana kuhusika na mauaji ya  Ndadaye mwaka wa 1993.

Tarehe 21 mwezi Oktoba kila mwaka huwa ni makumbusho ya kifo  cha Ndandaye  nchini Burundi.

Alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo na husherehekewa kama shujaa katika taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *