Aliyekuwa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga aaga dunia

Aliyekuwa Mbunge wa Kaloleni katika Kaunti ya Kilifi, Gunga Mwinga, amefariki.

Gunga ameaga dunia Jumapili alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Kibinafsi ya Mombasa.

Kulingana na taarifa, mbunge huyo wa zamani alikuwa akitibiwa hospitalini humo baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Gunga, ambaye ni wakili, alichaguliwa kama Mbunge wa Kaloleni mwaka wa 2013.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017, Gunga alipoteza kiti hicho kwa Paul Katana, ambaye ndiye mbunge wa sasa wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *