Alfred Bourgeois aliyehukumiwa kifo nchini Marekani auawa kwa sindano ya sumu

Mtu mmoja aliyemuua binti yake mchanga takriban miaka 20 iliyopita, amekuwa mfungwa wa pili kuuawa katika siku chache zilizopita nchini Marekani.

Kifo cha Alfred Bourgeois,aliyeuawa kwa kudungwa sindano ya sumu siku ya ijumaa kinajiri siku chache baada ya mfungwa mwengine kuuawa kwa njia hiyo hiyo baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama.’

Wafungwa wengine watatu wamepangiwa kuuawa kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kuhudumu cha rais Donald Trump tarehe 20 mwezi ujao.

Utekelezaji wa hukumu za kifo zilikuwa zimesitishwa nchini humo kwa muda wa miaka 17 kabla ya rais Trump kuagiza kurejelewa kwake mapema mwaka huu.

Iwapo hukumu za kifo cha wafungwa hao watatu zitatekelezwa,hiyo itakuwa idadi kubwa zaidi ya wafungwa waliouawa katika kipindi cha uongozi cha rais mmoja nchini humo.

Rais mteule Joe Biden ambaye atachukua hatamu za uongozi  nchini humo tarehe 20 mwezi ujao,amekuwa mpinzani mkubwa wa utekelezaji wa hukumu ya kifo nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *