Al-Shabaab washambulia kambi mbili za jeshi la taifa la Somalia

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameshambulia kambi mbili za jeshi la Somalia leo asubuhi.

Kambi hizo mbili zipo umbali wa kilomita 100 kusini magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Hussein Nur,ambaye ni afisa wa kijeshi, amesema wanajeshi kadhaa wameuawa kwenye mashambulizi hayo, yaliolenga kambi za za Bariire na Awdhigle.

Amesema serikali imewapeleka wanajeshi zaidi katika eneo hilo, ambapo wavamizi kadhaa wameauwa.

Kwa mujibu wa Nur, jeshi la Somalia sasa linadhibiti kambi hizo mbili pamoja na maeneo yaliyokaribu huku wakiwaandama magaidi hao.

Kundi hilo la kigaidi limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Kundi hilo la kigaidi la Al-Shabab ambalo linauhusiano na lile la  Al-Qaeda, limekuwa likitekeleza mashambulizi kwa miaka kadhaa huku likilenga kuanzisha sheria za kiislamu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *