AK Central Rift yalenga kuteua kikosi dhabiti cha chipukizi u 20

Chama cha riadha Kenya eneo la Central Rift kinapanga  kuteua timu dhabiti itakayoshiriki majaribio ya kitaifa ya timu ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.

Kulingana na mwenyekiti wa AK Central Rift Abraham Mutai ,wamekuwa wakiandaa kambi za wanariadha chipukizi ili kuwaandaa kwa majaribio ya kitaifa kutafuta timu ya Kenya itakayoshiriki mashindano ya dunia .

“Kwa sasa tumekuwa tukiandaa kambi kwa wanariadha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20  kila wakati wa likizo,tunataka kusema kuwa kama region tunataka kuhakiksha wanariadha wetu wamejiandaa vyema na wako katika hali nzuri kuishindia Kenya Nishani .Tutaandaa kambi ya mwisho mwezi April mwaka huu,lakini pia wanariadha wamekuwa wakifanya mazoezi”akasema Mutai

Mutai anajivunia matokeo bora ya wanariadha kutoka eneo hilo ambalo  wanariadha wake watano wanashikilia rekodi ya dunia kwa sasa huku wakilenga kuboresha matokeo yao.

“Tunajivunia kuwa na wanariadha tajika kutoka eneo langu na pia wanariadha watano wanaoshikilia rekodi za dunia wanatoka region yangu ,kwa sasa tuna miradi takriban 30 ya wanariadha inayoendelea kwa sasa  “akaongeza Mutai

Kenya itaandaa amshindano ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 katika uwanja wa Kasarani baina ya Agosti 17 na 22 mwaka huu.

Baadhi ya wanariadha kutoka Central Rift ni kama vile bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji Consenslus kipruto,Julius Yego na bingwa mara 7 wa dunia katika mita 3000 kuruka viunzi  na maji Ezekiel Kemboi miongoni mwa wengine.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *