Ajali nyingine yatokea Likoni Feri, masaa machache baada ya lori kutumbukia majini

Gari aina ya Pickup linalomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Ulinzi ya SGA limeanguka lilipokuwa likijaribu kuingia ndani ya feri katika Kivukio cha Likoni.

Hata hivyo, gari hilo limebahatika kutotumbukia ndani ya maji, huku dereva akiokolewa na kupelekwa hospitalini ili kutibiwa majeraha aliyopata.

Ajali hiyo imetokea masaa machache tu baada ya lori kutumbukia baharini katika sehemu iyo hiyo baada ya kukosa muelekeo lilipokuwa likielekea kwenye Feri ya MV Kilindini masaa ya alfajiri.

Lori hilo lilikuwa limebeba shehena ya vigae kutoka nchini Tanzania na lilikuwa linatarajiwa kuvuka kutoka Likoni kuelekea mjini Mombasa wakati ajali hiyo ilipotokea.

Lori laokolewa kutoka baharini baada ya kutumbukia leo alfajiri

 

Ajali hizo zimetokea siku mbili tu baada ya basi la kusafirisha watalii la Kampuni ya Pollman’s kukosa muelekeo na kutumbukia majini katika sehemu iyo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *