Aina mpya ya virusi vya Covid-19 yazidi kuripotiwa ughaibuni

Uhispania imedhibitisha visa vingine vinne vya maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona,ambavyo viligunduliwa hivi karibuni nchini Uingereza.

Maambukizi hayo yalionakiliwa mjini Madrid yanahusu watu ambao walizuru Uingereza hivi karibuni kulingana na maafisa wa afya mjini Madrid.

Ufaransa ,Denmark na Uholanzi pia zimeripoti visa kadha vya maambukizi ya virusi hivyo.

Wanasayansi wamesema kuwa aina hiyo mpya ya virusi husambaa kwa haraka lakini haimaanishi ni hatari kwa walioambukizwa.

Na nchini Japan, mji wa Tokyo umeshuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona,baada ya kuripotiwa kuzuka kwa aina mpya ya virusi vya ugonjwa huo nchini humo vinavyo sambaa kwa upesi huku serikali ikiwahimiza watu kusalia manyumbani kwao.

Visa vya maambukizi ya COVID-19 vimeongezeka hadi  949 mjini Tokyo wakati huu watu wanapotarajia kuukaribisha mwaka mpya.

Siku ya Ijumaa, Japan iliripoti kisa cha kwanza cha maambukizi ya aina hiyo mpya ya virusi vya Corona miongoni mwa abiria waliowasili kutoka Uingereza.

Aina hiyo mpya ya virusi viligunduliwa katika mtu mmoja aliyerejea nchini humo kutoka Uingereza.

Kufuatia msambao huo mpya serikali imeaagiza raia wa nchi hiyo kusalia manyumbani wako kwa hufo ya kusambaa zaidi kwa virusi hivyo.

Aina hiyo mpya ya virusi imesababisha hali ya wasi wasi nchini Afrika kusini,ambako waziri wa afya Zweli Mkhize alionya kuwa baadhi ya chipukizi ambao wamekuwa buheri wa afya hivi majuzi sasa wanajihisi wagonjwa baada ya kutangamana na wenzao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *