Categories
Michezo

Ahly watawazwa mabingwa wa Misri

Al Ahly walinyakua ubingwa wa  ligi kuu nchini Misri kwa mara ya 42 mwishoni mwa wiki iliyopita huku msimu ukikamilika .

Kocha wa Ahly Pitso Mosimane  aliendeleza matokeo bora  katika majukumu yake mapya na miamba hao wakiipiga  Talaea El Geish mabao 3-0 na kufunga msimu kwa pointi 89.

Walid Soliman , Geraldo na Mahmoud Kahraba walipachika mabao hayo ya Ahly  ambao wameshinda mechi 28 kati ya 34 walizocheza huku wakipiga sare  tano na kushindwa mchuano mmoja pekee.

Kwa jumla Ahly maarufu kama Red Devils wamefungwa mabao manane  na kuandikisha rekodi ya kuzoa pointi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja zikiwa 89.

Tanta, FC Masr na  Haras El Hodood  zimeshushwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza huku mabingwa wa msimu wa mwaka 1972 na 1973  Ghazl El Mahalla  wakipandishwa ngazi pamoja na Bank Al Ahly na Ceramica Cleopatra.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *