Ahly watawazwa mabingwa wa Misri
Al Ahly walinyakua ubingwa wa ligi kuu nchini Misri kwa mara ya 42 mwishoni mwa wiki iliyopita huku msimu ukikamilika .
Kocha wa Ahly Pitso Mosimane aliendeleza matokeo bora katika majukumu yake mapya na miamba hao wakiipiga Talaea El Geish mabao 3-0 na kufunga msimu kwa pointi 89.
Walid Soliman , Geraldo na Mahmoud Kahraba walipachika mabao hayo ya Ahly ambao wameshinda mechi 28 kati ya 34 walizocheza huku wakipiga sare tano na kushindwa mchuano mmoja pekee.
Kwa jumla Ahly maarufu kama Red Devils wamefungwa mabao manane na kuandikisha rekodi ya kuzoa pointi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja zikiwa 89.
Tanta, FC Masr na Haras El Hodood zimeshushwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza huku mabingwa wa msimu wa mwaka 1972 na 1973 Ghazl El Mahalla wakipandishwa ngazi pamoja na Bank Al Ahly na Ceramica Cleopatra.