Afrika Mashariki yakosa timu kwenya mataifa 24 ya AFCON mwaka ujao

Afrika mashiriki itakosa timu kwenye makala ya mwaka ujao ya fainali za kombe la AFCON baada ya waakilishi wote kushindwa kufuzu.

Uganda ilimaliza ya  tatu katika kundi B kwa pointi 8 nayo Burundi ikiwa ya mwisho kundini E,wakati Rwanda ikishikilia nafasi ya tatu katika kundi F kwa alama 5 nayo Kenya ni ya tatu katika kundi G kwa pointi 7.

Tanzania pia imeibuka ya tatu kundini J kwa alama 8.

Hata kutoka ukanda CECAFA kutakuwa na mwakilishi mmoja pekee ambaye ni Sudan baada ya kuibuka ya pili katika kundi  C.

Fainali za 33 za AFCON zitaandaliwa baina ya Januari na Februari mwaka ujao nchini Cameroon huku mataifa 24 yakishiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *