Categories
Habari

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma yazindua kitengo cha kushughulikia kesi za ufisadi.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma imeanzisha kitengo cha kushughulikia mashtaka ya kesi zinazohusu ufisadi pekee.

Afisi hiyo imesema kwamba kitengo hicho kipya kitaendeshwa na waendesha mashtaka wenye ujuzi wa hali ya juu na kiko chini ya Idara ya Uhalifu wa kiuchumi, Kimataifa na uhalifu ibuka (EIEC).

Kwenye taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma imeeleza kwamba kuanzishwa kwa kitengo hicho kumetokana na ugumu na pia utata kwenye kesi za ufisadi.

Afisi hiyo imesema kuwa hatua hiyo pia inajiri kutokana na matakwa ya umma kwenye vita dhidi ya ufisadi humu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *