AFC Leopards yamzindua Trucha kuwa kocha mpya kwa mkataba wa miaka miwili

Miamba wa soka nchini Afc Leopards mapema Jumatatu imemzindua Tomas Trucha kutoka Jamhuri ya Czech kuwa mkufunzi mpya kwa mkataba wa miaka miwili.

Trucha aliye na umri wa miaka 47 atasaidiwa na aliyekuwa kaimu kocha Athony Kimani .

Trucha ana leseni ya UEFA PRO na amefanya kazi ya ukufunzi katika timu kadhaa bara Afrika ,mara ya mwisho akiwa na kilabu  Township Rollers kutoka Botswana kuanzia Julai mwaka jana,akitokea   Orapa United pia ya Botswana mwaka 2018 .

Trucha akikaribishwa wa na mwenyekiti wa Leopards Dan Shikanda

Pia kocha huyo alikuwa na timu ya Fc  Tygerberg ya Afrika kusini mwaka 2012 kabla ya kujiunga na Capetown Fc katika wadhifa wa naibu kocha mwaka 2013.

Katika Jamhuri ya Czech Trucha amezinoa timu kadhaa ikiwemo kuwa naibu kocha wa vilabu vya Zbrojovka  Brno na Viktoria Plzen  mwaka 2017,naibu kocha wa Bohemians Fc mwaka 2016  na pia amewahi kuwa naibu kocha na afisa mkuu mtendaji wa timu ya Banik Ostrava mwaka 2012.

Jukumu kubwa kwa kocha anayerithi mikoboa ya ukufunzi wa Leopards kutoka kwa Andre Casa Mbungo wa Rwanda aliyeziuzulu kutokana na kutolipwa, ni kushinda kombe la ligi kuu ya Kenya ambalo Leopards walishinda kwa mara ya mwisho miaka 22 iliyopita huku msimu mpya ukianza rasmi tarehe 20 mwezi huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *