Madereva wasubiri kwa ghamu mashindano ya dunia ya Kenya

Huku mashindano ya dunia ya mbio za magari ulimwenguni yakisubiriwa kuandaliwa hapa nchini mwaka ujao,baada ya kuahirishwa kutoka Julai mwaka huu kutokana na Virusi vya Korona,Madereva mashuhuri wanayo matarajio mengi kuwa yatafana.

Wakizungumza maajuzi kupitia mtandao wa www.wrc.com  madereva wakongwe wanabashiri kuwa mashindano ya Kenya yatavutia sana mwaka ujao kutokana ,vivutio vingi vya utalii.

Mashindano ya dunia ya WRC yalirejeshwa kwenye kalenda ya kimataifa  kwa  mara ya kwanza baada ya Subira ya miaka 18 tangu yaondolewe .

Bingwa mara 9 wa dunia  Sebastian Loeb,ambaye ndiye dereva pekee ambaye aliwahishiriki mashindano hayo yalipoandaliwa Kenya mwaka 2002 kwa mara ya mwisho na kuibuka wa 6   amesema anayakumbuka vyema mashinadno ya Kenya  “kwangu mimi nina kumbukumbu nzuri za mashindano ya Kenya ,nilikuwa nikitazama nyani ,twiga na ndege za helicopters zikipaa  juu ya gari langu.

dereva Sebastien-Loeb

Bingwa mara 6 wa dunia  Sabastien Ogier anatarajiwa kushiriki mashindnao ya Kenya mwaka ujao na amedokeza kubatilisha azma yake ya kustaafu mwaka huu,ili ashiriki mashindano ya Kenya.

Ogier, ambaye huendesha gari aina ya  Toyota Gazoo alinyakua ubingwa wa mashindano hayo mwaka 2013, 2014, 2015, 2016, 2017 na  2018.

Sebastien-Ogier

Upande wake Tommi Mäkinen, ambaye ni dereva aliyenyakua ubingwa wa dunia mara 4 miaka ya 1996, 1997, 1998 na  1999 akiwa na gari aina ya  Mitsubishi Lancer Evolution, amesema anakumbuka vyema mashindano ya Kenya .

Dereva Tommi Makinnen.

Matayarisho kwa mashindano ya Kenya yanaendelea  vyema huku waandalizi wakisema kil kitu ki shwari.

Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa WRC Safari Rally, Phineas Kimathi ambaye ni dereva mstaafu amesema serikali imeekeza kikamilifu kwa mashindano hayo.

“Ningependa kuishukuru serikali kwa kujitolea na pia namshukuru waziri wa michezo Dr Amina Mohammed kwa uongozi bora ,tuna  kila usaidizi tunaohitajika’’akasema Kimathi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *