Categories
Michezo

Ahly waibwaga Wydad na kunusia fainali ya ligi ya mabingwa Afrika

Mabingwa mara nane wa taji ya ligi ya mabingwa Afrika Al Ahly walijiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali ya kombe hilo baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-0 ugenini mjini Casablanca dhidi ya wenyeji Wydad Casablanca.

Alhy maarufu kama Red Devils wanaofunzwa na Pitso Mosimane walianza mkondo huo wa kwanza wa semi fainali kwa makeke na matawi ya juu huku  Magdi Kafsha akifunga bao la kwanza kwa wageni kunako dakika ya 4 ya mchezo nayo wenyeji wakakosa penati iliyopigwa na Aouk Badi na kupanguliwa na kipa wa Ahly Mohammed

El Shanawy.

 

Wydad walionekana kupotea mchezoni katika kipindi cha pili ,wageni wakimiliki mpira kwa kipindi kirefu kabla Ali Malooul kufunga bao la pili  katika dakika ya 62 kupitia mkwaju wa penati.

Mkondo wa pili wa nusu fainali utasakatwa jijini Cairo Misri wikendi ijayo ambao Ahly wanahitaji tu sare au hata kupoteza kwa bao moja ili kutinga fainali,huku wakiwania taji ya 9.

Mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya pili kuchezwa Jumapili usiku,Raja Casablanca ya Moroko ikiwakaribisha vigogo wa Misri Zamalek,mechi ambapo itarushwa mbashara na Kbc channel 1 Tv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *