Meneja wa Mamelodi Sundowns Pitso Mosimane abwaga manyanga

Meneja wa mabingwa wa Afrika Kusini-kilabu ya Mamelodi Sundowns , Pitso Mosimane ametangaza kujiuzulu mapema leo.

Mosimane ambaye alitwaa ubingwa wa ligi kuu ya Afrika kusini kwa mara ya tano akiwa na timu hiyo maarufu kama the Brazilians msimu uliopita yuko njiani kujiunga na miamba wa Misri Al ahly .

Mosimane alianza kusakwa punde baada ya kushindi taji ya 10 ya ligi kuu Afrika kusini mwezi uliopita na ya tano mtawalia akiwa na Mamelodi .

Hata hivyo bado Mamelodi wana uwezo wa kukatalia mbali uhamisho wa Motsimane hadi Misri kulingana na kipengee katika mkataba wake.

Motsimane amekuwa na Mamelodi kwa miaka 8 ambapo amenyakua mataji 11 yakiwemo 5 mtawalia ya ligi kuu Afrika Kusini.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *