Wanyakuzi wa ardhi ya umma waagizwa kuirejesha kwa miradi ya maendeleo

Watu walionyakua maeneo yaliotengwa kwa matumizi ya umma wameagizwa kuhama ili kutoa fursa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kamishna wa kaunti ya Nairobi  Flora Mworoa alisema serikali imepanga kuzindua miradi mbali mbali katika kaunti ya Nairobi miongoni mwa uakarabati wa barabara,uzinduzi wa miradi ya maji na ile ya usafi  na haitaruhusu miradi hiyo kukwama kutokana na visa vya unyakuzi.

Akiongea wakati wa mkutano wa kamati ya ushirikishi wa utekelezaji wa miradi afisini mwake, afisa huyo wa utawala aliwahimiza wakazi wa Nairobi kuzingatia viwango vya juu vya usafi.

kamishna huyo wa kaunti aliwatahadharisha watu ambao wamekuwa wakitupa taka na chupa za plastiki kwenye mitaro katika maeneo yao ya makazi,akisema tabia hiyo imechangia kuziba kwa mitaro hiyo pamoja na kuchafua mazingira.

Mhandisi Andrew Maiteka wa halmasdhauri ya barabara kuu nchini alisema mkandarasi anayekarabati barabara kati ya  Kangundo na Kamulu amekumbana na changamoto nyingi kutokana na unyakuzi wa ardhi,jambo ambalo linatatiza ukarabati huo.

Aliongeza kuwa wanyakuzi hao lazima watimuliwe katika juhudi za kuzuia uharibifu wa barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *