Wanajeshi 100 wa Senegal waambukizwa Covid-19

Jeshi la Senegal limesema takribani wanajeshi wake 100 ambao walikuwa wakilinda amani nchini Gambia wameambukizwa virusi vya korona.

Wanajeshi hao ni miongoni mwa kikosi cha wanajeshi 600 ambao walirejea nyumbani.

Wamewekwa karantini katika sehemu ya Toubacouta, nchini humo karibu na mpaka wake na Gambia kama njia ya kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Waliothibitishwa kuwa na virusi hata hivyo hawana dalili huku upimaji zaidi ukiendelea.

Mpango wa kulinda amani nchini Gambia chini ya shirika la maendeleo magharibi mwa afrika, ECOWAS ulianzishwa mwaka wa 2012 na unajumuisha kwa wingi wanajeshi wa Senegal.

Wanajeshi walipelekwa nchini humo kumlazimisha aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh kakabidhi mamlaka kwa mrithi wake aliyechaguliwa Adama Barrow na kusaidia serikali mpya ya taifa hilo kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Muda wa kuhudumu wa kikosi hicho cha kulinda amani uliongezwa wakati wa mkutano wa mwisho wa ECOWAS kufuatia ombi la rais Barrow.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *