Uganda, nyumba ya msemaji wa serikali yashambuliwa

Maafisa wa Polisi nchini Uganda wanachunguza shambulizi kwenye nyumba ya msemaji wa serikali viungani mwa jiji la Kampala.

Ofwono Opondo alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba alikuwa ameshindwa kuwasiliana na familia yake iliyovamiwa nyumbani kwake.

Opondo aliwaambia wanahabari kwamba watu wengi waliingia kwa nguvu nyumbani kwake na kuizuilia familia yake ndani ya chumba kimoja cha kulala wakati wakipekua vyumba vingine.

Naibu Msemaji wa Polisi Polly Namaye, alithibitisha uvamizi huyo akisema familia hiyo ilikuwa salama hata ingawa walishtuka sana. Alisema polisi wanawasaka wavamizi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *