Nigeria, wanaume wabakaji kuhasiwa

Bunge la jimbo la Kaduna, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria limeidhinisha kuhasiwa kwa wanaume wote watakaopatikana na hatia ya ubakaji.

Kamishna wa jimbo hilo anayehusika na masuala ya wanawake na ustawi wa kijamii, Hafsat Baba, alisifia hatua hiyo akisema itakomesha vitendo vya ubakaji.

Gavana wa jimbo hilo, Nasir Ahmad el-Rufai, sasa atahitajika kutia sahihi mswada huo ili kuufanya kuwa sheria.

Mnamo mwezi Juni, magavana nchini Nigeria walitangaza hali ya hatari kuhusiana na ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake na watoto nchini humo.

Idadi ya watu wanaohukumiwa kuhusiana na ubakaji nchini Nigeria bado ni ya chini mno na unyanyapaa huwafanya waathiriwa kusita kuripoti visa hivyo kwa maafisa wa usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *