Mwakilishi wadi akamatwa kwa kumjeruhi mwanamke kaunti ndogo ya Endebes

Maafisa wa polisi katika kaunti ndogo ya Endebes wamemtia nguvuni mwakilishi wadi mmoja na dadake kwa kumpiga mwanamke mmoja waliomshtumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba yao.

OCPD wa Endebess Salesioh Murithi alisema tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Cholim ambapo washukiwa hao pamoja na jamaa wengine wa familia walipokwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kabla ya kumpiga pamoja na mtoto wake wa kiume.

Kulingana na ripoti za polisi,Trikoi Kapchanga na jamaa wengine 10 wa familia walienda nyumbani kwa Justin Chepkwarat ambapo walimpiga akiwa na mwanawe Gideon Naibei mwenye umri wa miaka 23.

OCPD huyo  alidhibitisha kuwa  MCA huyo pamoja na dadake Hellen Kapchanga walitiwa nguvuni huku wenzao 8 wakisakwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *