Muigizaji maarufu wa Mombasa Pretty Mutave aaga dunia

Muigizaji maarufu wa Mombasa kwa jina Pretty Mutave ameaga dunia mapema leo asubuhi akielekea hospitali ya Coast General kupata matibabu.

Ripoti zinaonyesha kwamba Pretty ambaye aliwahi kuigiza kama Waridi kwenye kipindi Moyo, akaigiza kama Dee kwenye Aziza na kama Zari kwenye maza amekuwa akiugua tangu mwezi machi mwaka huu.

Waigizaji wenzake wameandika kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha masikitiko kutokana na kifo chake Pretty.

 

Mtangazaji Rashid Abdalla ambaye pia ana kampuni ya kutayarisha vipindi naye amemkumbuka Pretty kupitia ukurasa wake wa facebook.

“#sisemikitu Japo kazi ya Mungu haina makosa lakini msiba hauna mazoea. Pretty Mutave kipaji chako kikawe nuru kwa malaika. Mola ailaze roho yako pema peponi inshallah. Heshima na kipaji chako vitadumu milele.” Aliandika Rashid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *