Mkenya Elsa Majimbo kufanya kazi na FENTY ya Rihanna

Mchekeshaji mkenya wa miaka 19 Bi. Elsa Majimbo ametia saini mkataba na kampuni ya mwanamziki mashuhuri ulimwenguni Rihanna iitwayo FENTY BEAUTY.

Chini ya mkataba huo Elsa atahitajika kuonyesha miwani mbali mbali inayotengenezwa na kampuni hiyo ya Rihanna na kisha kulipwa. Ni kazi ya mauzo haswa.

Majimbo kupitia twitter siku ya jumapili alitangaza kwamba, “Mimi wa miaka 19 nimepata fursa ya kufanya kazi na @FentyOfficial. Najivunia”

Siku hiyo hiyo ya jumapili, Rihanna kupitia ukurasa wa twitter wa kampuni ya Fenty ali share video ya Elsa akisema, “Shughuli za wikendi na mchekeshaji mkenya @ElsaAngel19 akiwa amevalia kila aina ya FENTY. Jumapili njema kila mmoja!”

 

Bi. Elsa akiwa amevalia miwani ya FENTY

Kwenye hiyo video Elsa anabadilisha badilisha miwani iliyoundwa na FENTY huku akisifia Rihanna na kampuni ya FENTY.

 

Elsa ni kati ya wachekeshaji na wasanii kadhaa wakenya ambao hutengeneza video za vichekesho na burudani na kuziachia kwenye mitandao ya kijamii. Video za Elsa hupendelewa na watu wengi kiasi cha kufikisha mitazamo au ukipenda views laki tatu.

Hii sio kazi ya kwanza ambayo Elsa amepata kutokana na kazi zake za uchekeshaji. Aliwahi kupata kazi ya mauzo na kampuni ya vipodozi ya MAC Africa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *