Kupungua kwa visa vya Covid-19 nchini kunatokana na idadi ndogo ya sampuli zinazopimwa

Mkurugenzi wa afya kwa umma  Dkt. Francis Kuria amesema kuwa kupungua kwa idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa  COVID-19 kunatokana na kupungua kwa idadi ya sampuli zinazopimwa.

Pungua kwa sampuli zinazopimwa kunatokana na uhaba wa kemikali zinazohitajika wakati wa kupima sampuli hizo ambazo zinahitajika kote duniani.

Alisema Kenya tayari imeagiza kemikali zaidi ambazo zinatarajiwa nchini mwisho wa juma hili.

Dkt. Kuria aliwaonya wakenya  dhidi ya kulegeza maagizo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona kwa dhana kuwa maambukizi hayo yanaopungua nchini.

Aliongeza kuwa maambukizi hayo bado hayajakabiliwa nchini huku akiwahimiza wakenya kuzingatia maagizo ya kukabiliana na virusi hivyo.

Dkt. Kuria alisema idadi ya wanaolazwa hospitalini bado ni ya chini lakini ugonjwa wa COVID-19 bado ni tisho.

Kwa mujibu wa Dkt Kuria wahasiriwa saba kati ya kumi waliofariki kutokana na ugonjwa huo hawakua wakiugua maradhi mengine.

Aliwahimiza wakenya kujiepusha na mikutano ili wasiambukizwe ugonjwa wa Covid-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *