Ken Lusaka atakiwa kumakinika zaidi katika majukumu yake ya spika wa Senate

Maseneta siku ya Jumanne walitoa changamoto kwa spika  Ken Lusaka kuongoza bunge hilo ipasavyo na kushughulikia miswada yote kwa wakati uliowekwa.

Maseneta hao walisema kuwa kuna miswada mingi ambayo haijashughulikiwa na bunge hilo na ilhali muda unayoyoma.

Seneta wa kaunti ya  Makueni Mutula Kilonza Junior alisema kuwa iwapo mikakati mwafaka haitawekwa ili kuhakikisha kuwa bunge la  Senate linatekeleza ipasavyo majukumu yake, itakuwa vigumu kwa maseneta kuhudhuria vikao mwaka ujao kutokana na kampeini za mapema.

Akichangia kwa hoja ya kurekebisha ratiba ya bunge la Senate ili kuruhusu bunge hilo kuwa na vikao vitatu kwa wiki, seneta wa kaunti ya  Makueni alisema kuwa kwa vile kumekuwa na ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa bunge hilo na serikali, spika anapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha kuwa bunge hilo linatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mswada huo wa marekebisho uliwasilishwa na seneta wa kaunti ya Wajir  Abdulahi Ali.

Kwa sasa, bunge la  Senate limerekebisha kalenda yake na kuwaruhusu maseneta kuwa na vikao siku za jummanne na alhamisi.

Hata hivyo wengi wanahisi kuwa siku hizo mbili kwa wiki hazitoshi kutekeleza ipasavyo majukumu ya bunge hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *