Jamii ya kimataifa yatakiwa kuangazia habari njema kutoka Afrika

Bara la afrika lina uwezo mkubwa na fursa nyingi katika kila sekta ambazo zinastahili kutumika,haya ni kwa mujibu wa aliyekuwa naibu wa spika wa bunge la Israel Hilik Bar.

Bar ametoa wito kwa jamii ya kimataifa na vyombo vya habari kuangazia habari njema kutoka bara la Afrika.

Naibu huyo spika wa zamani aliuambia mkutano wa kimataifa wa Webinar kuhusu uongozi kwamba, vyombo vya habari havipaswi kuzingatia tu habari za ufisadi,umaskini na ghasia barani afrika.

Alisema vyombo hivyo vinapaswa kuangazia fursa zilizoko barani Afrika.

Aliongeza kwamba bara la afrika linapaswa kusaidiwa kutimiza uwezo wake kupitia biashara na uvumbuzi na siyo kupitia misaada.

Akiongea,rais wa bunge la Niger Tinni Ousseini, alisema kuwa janga la corona limetoa fursa kwa bara hili kutekeleza marekebisho katika sekta zote.

Alisema jamii ya kimataifa inaweza kupunguza utoaji wa gesi ya sumu ya Carbon dioxide kwa kupunguza safari za ndege.

Rebecca Kadaga, Spika wa bunge la Uganda alitoa wito kwa wabunge kuzindua sera zinazochochea utafiti na uvumbuzi katika matumizi ya rasli mali za bara hili.

Mkutano huo uliandaliwa na wakfu wa amani wa Universal unaofadhiliwa na Dr Hak Ja Han Moon.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *