Zaidi ya watu elfu 13 wakiwemo wafuasi wa upinzani wanyongwa gerezani Syria

Watu wapitao elfu 13 wengi wao wakiwaA� wafuasi wa upinzani wamenyongwa katika gereza la siri nchini Syria kwa mujibu wa shirika laA� Amnesty International. Ripoti mpya ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu inadai kuwepo kwa misururu ya watu kunyongwa kila juma katika gereza la Saydnaya baina ya mwezi Septemba mwaka wa 2011 na Disemba mwaka wa 2015. Shirika hilo la Amnesty linadai kuwa hatua ya kunyongwa kwa wafungwa hao iliamrishwa na maafisa wakuu wa serikali ya Syria.A� Shirika hilo lilihoji watu wakiwemo waliokuwa walinzi, wafungwa na maafisa wa magereza.A� Inadaiwa kuwa kila wiki au mara mbili kwa wiki watu kati ya 20 na 50 walikuwa wakinyongwa katika gereza hilo lililoko kaskazini mwa Damascus.