Zaidi ya watu 500 wafariki kutokana na mchamko wa kipindupindu DRC

Zaidi ya watu 500 wamefariki dunia kutokana na mchamko wa maradhi ya kipindupindu katika Jamhuri ya demokrasia ya Congo. Kuingana na shirika la afya duniani-WHO ugonjwa huo tayari umegunduliwa katika sehemu 10 za mijini, ukiwemo mji mkuu Kinshasa. Mkasa huo umeibua wasi wasi mkubwa hasa katika eneo la kati la Kasai, ambakoA�A� mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamewakosesha makao zaidi ya raiaA� milioni 1.4.Ugonjwa wa kipindupindu hutokea mara kwa mara katika nchi hiyo kutokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa. Kwa mujibu wa shirika la WHO takriban watu 528 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo ambao umeenea katikaA� majimbo 20 kati ya majimbo 26 ya taifa hilo. Shirika hilo la afya duniani limewapeleka wataalamu wake wa afya na maafisa wa afya ya umma katika nchi hiyo ili kukomesha kusambaa kwa ugonjwa huo.