Zaidi ya watu 300 wafariki katika maporomokoya ardhi Sierra Leone

Zaidi ya watu mia tatu wameuawa katika maporomoko ya ardhi na mafuriko karibu na mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown. Eneo moja la mlima liliporomoka katika eneo la Regent mapema hapo jana kufuatia mvua kubwa na kuacha nyumba kadhaa zimefunikwa na matope.A� Mashahidi mahala hapo walisema kuwa waathiriwa wengi walikuwa wamelala wakati kisa hicho kilipotokea.A� Idadi ya waathiriwa inatarajiwa kuongezeka.