Zaidi Ya Maafisa 300 Wa Polisi Waachishwa Kazi

Zaidi ya maafisa 300 wa polisi wameachishwa kazi kwa kukataa kushirikiana na Bodi ya ukaguzi ya huduma ya polisi. Maafisa hao hawakufika mbele ya Bodi hiyo wala kutoa stakabadhi walizohitajika kuwasilisha kwa ukaguzi wao. Maafisa wanaohusika ni wale wanaohudumu katika vyeo vya Senior Inspekta na koplo na watapewa barua za kuachishwa kazi na Isnpekta Jenerali wa polisi katika siku chache zijazo. Hta hivyo maafisa hao wamepewa nafasi ya kukata rufani kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na Tume ya huduma za polisi. Hatua ya kuwaachisha kazi ilichukuliwa baada ya kuibuka kwamba wameanza mbinu ya kulaghai watu pesa walipogundua kwamba huenda wakaachishwa kazi. Tume ya huduma za polisi imewasilisha barua zao kwa Inspekta jenerali wa polisi. Mwenyekiti wa tume hiyo Johnstone Kavuludi anaongoza mpango huo wa ukaguzi wa siku 10 kwa maafisa wa polisi wa trafiki katika eneo la magharibi mwa nchi.