Yego atarajia kupona jeraha kabla ya mashindano ya Jumuiya ya Madola

Bingwa wa dunia wa urushaji sagai mwaka 2015, Julius Yego anatarajia kupona jeraha la paja kabla ya kuandaliwa kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka ujao. Yego alisema hayo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kikosi cha Kenya kilichoshiriki katika mashindano ya riadha duniani kiliporejeaA� nyumbani kutoka jijini London walikomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya washindi Marekani. YegoA�A� alipokonywa na Johannes Vetter wa Ujerumani taji aliyotwaaA� miaka miwili iliyopita nchini Uchina; baada ya kurusha sagai mara mbili na kumaliza katika nafasi ya 13, fainalini. Yego amesema atatafuta tiba mjarabu ya jeraha linalomsumbua ambalo alisema nusra litatize matokeo yake katika michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2014, lakini akahimili na kunyakua nishani ya dhahabu. Aidha, jeraha hilo lilimtatiza kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio mwaka jana mbali na kwamba alikuwa wa pili.A� Wakati uo huo, bingwa wa dunia mwaka huu katika mbio za mita 1500, Elijah Manangoi, amesema ananuia kuuboresha muda wake kabla ya mwisho wa msimu huu, huku lengo lake kuu likiwa kuvunja rekodi ya mbio hizo iliyoandikishwa na Hicham El Gouraj wa Moroko miaka 19 iliyopita. Kenya ilimaliza ya pili kwa jumla ya nishani 12,A� Tano za Dhahabu, mbili za fedha na tano za shaba, matokeo finyu yakilinganishwa na ya mwaka 2015 ambapo Kenya iliongoza duniani kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo.