Yaya Toure Kurejea Mazoezini

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure alirejea mazoezini na anatarajiwa kuchezaA� katika mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya kombe la kilabu bingwa Barani Ulaya dhidi ya Real Madrid leo usiku. Toure mzaliwa wa Kodivaa hakuichezea CityA� mechi mbili zilizopita ikiwemo mechi ya mkondo wa kwanza wakati City ilipotoka sare kappa na Madrid juma lililopita kutokana na jeraha pajani. Kiungo wa Uingereza David Silva hatashirikiA� katika mechi hiyo baada ya kujeruhiwa mguuni wakati wa mechi ya mkondo wa kwanza. City pia itazikosa huduma za kiungo wa Ufaransa Samir Nasri. Wakati uo huo, kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Cristiano Ronaldo amepata nafuu na atacheza nusu fainali mkondo wa pili dhidi ya Manchester City. Ronaldo hakucheza mechi ya mkondo wa kwanza walipotoka sare kapa kutokana na jeraha pajani lakini alirejea mazoezini Jumatatu na Jumanne. Hata hivyo Zidane alithibitisha kuwa Madrid itazikosa huduma za mshambulizi Karim Benzema na kiungo Casemiro wanaouguza jeraha.