Wizara ya fedha kutoa mikopo kwa serikali za kaunti

Wizara ya fedha itatoa mikopo kwa serikali za kaunti zinazohitaji fedha kwa dharura na hazina fedha zozote katika akaunti zao. Hii itawezesha serikali za kaunti kupokea mikopo yenye masharti nafuu ambayo haina masharti ghali ya mikopo kama ile inayotolewa na benki za humu nchini. Wizara ya fedha kisha itakata fedha hizo za mikopo kwenye fedha ambazo hutengewa kaunti kila mwaka. Hatua hii iliidhinishwa kwenye mkutano wa baraza laA� masuala ya bajeti na kiuchumi la viwango viwili vya serikali lililoongozwa na naibu wa rais William Ruto katika makazi yake yalioko mtaa wa Karen jijini Nairobi.Waziri wa fedha Henry Rotich alisema baada ya kushauriana na banki kuu utaratibu wa kukabidhi kaunti fedha hizo uliafikiwa. Rotich pia alitangaza kwamba wafadhili wamekabidhi serikali shilingi bilioni 5.5 za kufanya mageuzi katika sekta za afya, kilimo na muundo msingi wa kaunti.Mkutano huo uliwajumuisha magavana, maafisa wa kuaunti, mawaziri, makatibu, maafisa wa tume ya ugavi wa mapato, bunge na msimamizi wa bajeti.