Wizara Ya Fedha Afrika Kusini Yapendekeza Rais Jacob Zuma Arejeshe Kwa Serikali Takriban Dola Laki Tano Pamoja Na Milioni 23 Pesa Za Umma

Wizara ya fedha nchini Afrika kusini imependekeza kuwa rais  Jacob Zuma arejeshe kwa serikali takriban dola laki tano alizotumia kukarabati makazi yake ya kibinafsi.  Haya yanawadia baada ya mahakama ya juu nchini humo mapema mwaka huu kuamua kuwa rais  Zuma arejeshe dola milioni 23 za pesa za umma alizotumia kukarabati makazi yake mwaka wa 2009. Zuma anatarajiwa kulipa pesa hizo kwa muda wa siku  45.  Mnamo mwezi Machi mwaka huu mahakama ya kikatiba iliipa hazina kuu miezi miwili kubaini kiwango cha pesa ambacho Zuma alitakikana kulipa. Chama kikuu cha upinzani cha  Democratic Alliance kiliunga mkono ripoti hiyo ya hazina kuu. Makazi hayo ya Zuma yalijengwa katika eneo la  Nkandla katika jimbo la  KwaZulu-Natal.