Willy Mtengo Aidhinishwa Kugombea Eneo Bunge la Malindi

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imemruhusu mgombezi wa chama cha ODM Willy Mtengo kugombea uchaguzi mdogo wa kiti cha eneo bunge la Malindi.Mtengo ambaye alikuwa ameandamana na magavana Amason Kingi na Hassan Joho aliidhinishwa kugombea kiti hicho licha ya madai kwamba makaratasi yake hayakuwa sawa.Mgombezi wa chama cha Jubilee Alliance Phillip Charo vile vile ameidhinishwa kugombe uchaguzi huo mdogo.