Ruto ampigia debe Sonko kuwania Ugavana

Naibu RaisA� William Ruto amehimiza wanasiasa wote wa Jubilee katika Kaunti ya Nairobi, kuungana na kumuunga mkono Seneta Mike Sonko, anapomenyana na wawaniaji wengine wawili kwa wadhifa wa Gavana wa Jiji hilo. Sonko alikabidhiwa hati ya uteuzi wa chama hicho cha Jubilee jana, na wakati huo huo kumtaja mgombea mwenzaA� ambaye ni mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni ya vivo energy , Polycap Igathe. Wawili hao walielezea matumaini yao ya kurejesha Jiji la Nairobi katika fahari yake ya hapo awali. Sonko aliahidi kuboresha uadilifu katika utoaji huduma iwapo atachaguliwa. Katika Kaunti ya Embu, Gavana Martin Wambora amemteuwa mfanyibiashara mmoja wa eneo hilo David Kariuki, kuwa mgombea mwenza, anapojitahidi kutetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha Jubilee; wiki mbili baada ya kushinda uchaguzi wa mchujo wa chama hicho. Kwingineko, baadhi ya wawaniaji wa chama cha Amani National Congress, katika eneo-bunge la Dagoretti Kaskazini, wamejitenga na shughuli ya uteuzi katika chama hichoA� ambayo iliandaliwa leo,A� wakisema kwamba hawakuruhusiwa kushiriki. Wamedai shughuli hiyo iliandaliwa kwa haraka,A� huku wakimshtumu kiongozi wa chama hicho Musalia Mudavadi kwa kumpendelea mmoja wa wawaniaji.