Wetangula Atakiwa Kuwasilisha Habari Kuhusu Mauwaji Ya Mfanyibiashara Jacob Juma

Inspekta Jenerali wa polisi Joseph Boinnet amemtaka seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula kuwasilisha kwa polisi habari aliyo nayo kuhusiana na mauaji ya mfanyibiashara matata Jacob Juma. Haya yamejiri baada ya Wetangula kudai kuwa anajua majina ya watu waliomuua Juma baada ya mfanyibiashsra huyo kufichua majina hayo kwake huku akisema kuwa atataja majina hayo wakati wa mazishi ya Juma jumamosi ijayo. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Boinet alisema anatarajia kuwa Wetangula ambaye ni wakili wa kutajika na ambaye amehudumia taifa hili katika nyadhifa mbalimbali ana uwezo wa kupambanua ukweli na uongo na hivyo kama anao ukweli anapaswa kuutoa kwa polisi ili kuwawezesha kuchukua hatua mwafaka. Wananchi watapata mafasi ya kutazama mwili wa Juma hapo kesho katika bustani ya Uhuru. Juma aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 6 mwezi huu alipokuwa akielekea nyumbani kwake katika eneo la Karen jijini Nairobi.

A�