Wetangula Amtuhumu Mkeo Kwa Madai Ya Dhuluma

Kisa ambapo seneta wa Bungoma Moses Wetanga��ula amedai kuwa mkewe alimdhulumu huenda kisichunguzwe kwani seneta huyo hajaandikisha taarifa kwa polisi. Wetangula anataka mkewe Ann achukuliwe hatua kwa madai ya kumjeruhi. Hata hivyo mkewe pia aliwasilisha malalamishi kwa polisi akidai kuwa Wetangula alimdhulumu. Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya Nairobi Japheth Koome amesema polisi wanafanya uchunguzi kuhusu visa hivyo viwili. Hata hivyo, uchunguzi wa polisi hauwezi kukamilika hadi pale Wetangula na mkewe Ann watakapoandikisha taarifa kwa polisi. Ann Wetangula alikuwa wa kwanza kudai kuwa mumewe alimdhulumu mnamo tarehe-21 mwezi Februari mwaka huu. Na baadaye siku hiyo hiyo, Wetangula aliwasilisha malalamishi kwenye kituo cha polisi cha Langa��ata akidai kuwa mkewe alimdhulumu. Wetangula alidai kwamba mkewe alipandwa na mori alipomshutumu kwa uzinzi ndiposa akamshambulia. Seneta huyo alidai mkewe alimjeruhi kichwani, mkono wa kushoto, mguu wa kushoto na kifuani. Aidha aliwasilisha ripoti ya daktari kuthibitisha majeraha hayo.