Wetangula ajibu shtuma za kiongozi wa ODM kuhusiana na madai ya kuendeleza uhasama wa kibinafsi

Kiongozi wa chama cha FORD-Kenya, Moses Wetangula amejibu shutma za kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuhusiana na madai ya kuendeleza uhasama wa kibinafsi. Wetangula amedai kwamba Raila ameghubikwa na mgogoro wa kisiasa, na hapaswi kutambuliwa kuwa mmoja wa vinara wa Uhuru Kenyattamuungano wa NASA baada ya kauznisha ushirikiano mpya na Rais Uhuru Kenyatta. Siku ya Jumanne, hatibu wa ofisi ya Raila Odinga Dennis Onyang, alitoa taarifa ya kumtahadharisha Wetangula aache kumshtumu kiongozi huyo wa ODM eti alichochea kuondolewa kwake kama kiongpzi wa walio wachaceh katika Bunge la Seneti. Katika taarifa iliyokuwa mna matamshi makali, Odinga alimshtumu Wetangula kwa kuto-zingatia ukweli, kujihusisha na mambo ya upuuzi, lakini Wetangula hangenyamaa bila kutoa jawabu lake.