Waziri wa kigeni Amina Mohammed atuzwa kwa kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Japan

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni balozi Amina Mohammed ametunukiwa tuzo la Grand Cordon of the Order of the Rising Sun katika makao ya kifalme mjini Tokyo na mfalme wa Japan Akihito. Hiyo ndiyo A�tuzo ya juu kabisa ambayo hukabidhiwa raia wa kigeni kwa utambuzi wa ufanisi walioafikia. Balozi A�Amina alikabidhiwa tuzo hiyo kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya Kenya na Japan. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Amina alimshukuru mfalme Akihito, raia na serikali ya Japan kwa kumtunukia tuzo hiyo akiongeza kusema kwamba uhusiano kati ya Kenya na Japan ni dhabiti A�na unatarajiwa kukuzwa hata zaidi. Amina alitekeleza A�wajibu muhimu katika kufanikisha mkutano wa kimataifa wa sita wa Tokyo kuhusu maendeleo barani Afrika ulioandaliwa jijini Nairobi mwezi Agosti mwaka uliopita ambapo mkutano huo uliandaliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika.