Waziri wa habari Tanzania Nnauye aanzisha uchunguzi kufuatia uvamizi wa kituo cha runinga

Waziri wa habari nchini Tanzania, Nape Nnauye amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na madai ya uvamizi wa kituo kimoja cha runinga na afisa wa serikali. Kamera za CCTV zilionesha mrakibu wa jiji la Dar es Salaam, Paul Makonda, akiandamana na maafisa wa polisi wakiingia katika studio za kituo cha runinga cha Clouds Media Ijumaa usiku. Watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii walitaka Makonda achukuliwe hatua za kinidhamu. Ilidaiwa kuwa Makonda hakufurahishwa na hatua ya kituo hicho ya kukosa kupeperusha habari ambayo ingemdhalalisha mhubiri mmoja ambaye alikuwa ametofautiana naye kuhusu sakata ya ulanguzi wa mihadarati.