Waziri wa fedha, Rotich alihimiza bunge kubadili sheria inayodhibiti viwango vya riba za mikopo

Waziri wa fedha,Henry Rotich kwa mara nyingine amelihimiza bunge kubadili sheria inayodhibiti viwango vya riba za mikopo ili sekta ya kibinafsi iweze kunufaika na mikopo. Rotich amesema ajenda kuu nne za serikali ya Jubilee zitaafikiwa kutokana na msukumo wa sekta ya kibinafsi ambayo kwa sasa haipokei mikopo kutoka benki. Kenya ilithibiti viwango vya riba mwaka mmoja unusu uliopita. Kufuatia hatua hiyo benki zilipunguza mikopo inayotolewa kwa sekta ya kibinafsi. A�Wakati huo huo nchi ya Japan inanuia kuwekeza shilingi bilioni-40 katika miradi kadhaa ya muundo msingi ili kufanikisha ajenda nne kuu za serikali. Pesa hizo zitafadhili miradi ya upanuzi wa bandari ya Mombasa na ujenzi wa barabara ya kando ya Dongo Kundu miongoni mwa miradi mingine.