Waziri Wa Elimu, Matiang’i Asema Serikali Haitasaidia Kujega Shule Zilizoharibiwa Na Wanafunzi

Waziri wa elimu Fred Matianga��i amewaagiza walimu wakuu wa shule kutowasajili wanafunzi wanaohamishwa kutoka shule zilizokumbwa na maandamano ya wanafunzi bila barua ya idhini kutoka kwa wakurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo. Akiongea katika taasisi ya kubuni mitaala hapa nchini KICD waziri alisema serikali haitasaidia kujenga upya shule zinazoharibiwa na wanafunzi . Amesema wanafunzi wanaohusika katika vitendo vya aina hiyo watalipia uharibifu wote unaotokea.
Hayo yamejiri siku moja baada ya wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Itierio kaunti ya Kisii kuchoma mabweni saba baada ya kudaiwa kunyimwa fursa ya kutazama mechi ya soka kati ya Ureno na Croatia kwenye mechi zinazoendelea za Euro 2016 . Shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana . Kisa hicho cha hivi punde ni moja wapo ya visa vya machafuko kuzuka katika shule za upili ambavyo vimesababisha kuchomwa kwa zaidi ya shule 20 katika muda wa miezi mitatu iliyopita.