Waziri Wa Afya Ubelgiji Ahofia Ongezeko La Waliofariki kutokana Na Mashambulizi

Waziri wa afya nchini Ubelgiji Maggie de Block amesema kuwa watu kadhaa wangali katika chumba cha wagojnwa mahututi kufuatia mashambulizi ya bomu yaliyotokea jijini Brussels na kusababisha vifo vya watu wapatao 31. Block alisema kuwa watu wapatao 300 walijeruhiwa huku wengine 61 wakisalia katika hali mahututi huku akisema kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka. Mapema viongozi wa mashtaka walidhibitisha kuwa walikuwa wamewatambua wawili kati ya wavamizi wanne waliotekeleza shambulizi hilo kuwa kaka wawili Khalid na Brahim el-Bakraoui. Inaaminika kuwa mmoja wa washambulizi hao alifariki na mwingine akatoroka.