Waziri Mkuu Wa India Narendra Modi Akaribishwa Katika Ikulu Ya Nairobi

RaisA�A�Uhuru Kenyatta leo asubuhi alimlaki rasmi waziri mkuu wa India anayezuru hapa nchini,A�Narendra Modi katika ikulu ya Nairobi ambapo alipigiwa mizinga-19. Narendra aliwasili hapa nchini jana alasiri na kuelekea katika uwanja wa michezo wa Safaricom, Kasarani ambako yeye na rais Uhuru Kenyatta walihutubia jamii ya Wahindi hapa nchini. Leo asubuhi Narendra aliye na kwenye mkondo wa mwisho wa ziara yake hapa nchini aliweka shada la maua kwenye kaburi la hayati Mzee Jomo Kenyatta kwenye majengo ya Bunge. Baadaye alielekea katika ikulu kwa makarabisho rasmi. Na baadaye katika ikulu ya Nairobi, viongozi hao wawili wataongoza jumbe zao katika mazungumzo ya pande mbili. Rais Kenyatta naA�Narendra wataandaa kikao cha pamoja cha wanahabari kabla ya kuhutubia kongamano la kibiashara kati ya Kenya na India baadaye alasiri. Ziara hiyo ya Narendra inatarajiwa kuimarisha biashara kati ya Kenya na India kwa kupunguza nakisi ya kibiashara iliyoko baina ya nchi hizo mbili. Ziara yake hapa nchini ni mojawapo ya ziara za viongozi mashuhuri wa kigeni waliozuru hapa nchini katika siku za hivi majuzi.