Waziri Mkuu Wa India Kuzuru Marekani

Rais Donald Trump amemwalika Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kuzuru Marekani baada ya mawasiliano kati ya viongozi hao wawili. Marekani inasema inaichukulia India kuwa rafiki wa kweli na mshirika katika juhudi za kukabiliana na changamoto za dunia.Wawili hao walijadili fursa za kuimarisha ushirikiano baina ya India na Marekani hasa katika maswala ya uchumi na ulinzi.