Waziri Mkuu Libya ataka silaha ya umoja wa mataifa dhidi yao kuondolewa

Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj amemuambia waziri wa ulinzi wa Amerika A�Jim Mattis kuwa anatumai A�marufuku ya silaha ya umoja wa mataifa dhidi ya nchi hiyo itaondolewa.Umoja wa mataifa ulitangaza marufuku hiyo mwaka wa 2011 wakati wa maasi yaliotimua utawala wa rais Moamer Kadhafi.Wakati wa mkutano katika makao makuu ya kijeshi ya Pantagon nchini Amerika,Sarraj alimuambia Mattis kwamba Libya imepata mafanikio makubwa kwenye jitihada zake A�dhidi ya wanamgambo wa kiislamu pamoja na kundi la kigaidi la ISIS.Serikali ya kitaifa ya Sarraj inayoungwa mkono na umoja wa mataifa imekuwa na changamoto kubwa kudumisha utawala wake nchini Libya kutokana na upinzani mkali kutoka kwa serikali nyingine mashariki mwa nchi hiyo inayoungwa na mbabe wa kivita Khalifa Haftar. Sarraj anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump mjini Washington hii leo.